TAARIFA KWA UMMA
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana
na matamshi yaliyotolewa na Leonard Swai, Wakili wa TAKUKURU aliyenukuliwa
kwenye vyombo vya Habari tarehe 15/4/2016 kuhusiana na hali ya Rushwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wakili huyo alinukuliwa akisema kuwa “Kuna Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu” baada ya kutolewa hukumu ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO
Bw. William Mhando ambaye alionekana hana hatia.
Wakili
Leonard Swai si msemaji Rasmi wa Taasisi hivyo matamshi aliyoyatoa si msimamo
wa TAKUKURU kuhusu Mahakama. Tunaiomba Idara ya Mahakama na jamii kwa ujumla
itambue kuwa matamshi hayo aliyoyatoa ni maoni yake binafsi.
TAKUKURU
ina jukumu la kisheria la Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mahakama ni muhimili
wa Serikali unaotoa haki. Tunaamini kila Taasisi itaendelea kutekeleza majukumu
yake kwa kufuata miongozo ya Sheria zilizopo.
TAKUKURU
inaheshimu uhuru na mamlaka ya Mahakama na itaendelea kufanya hivyo katika
utekelezaji wa majukumu yake.
IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO,
TAKUKURU
MAKAO MAKUU
20 April, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...