TAASISI isiyo ya kiserikali T-MARC Tanzania imezindua rasmi jengo lake jipya pamoja na ghala maalum la kisasa litakalotumika kuhifadhia bidhaa zao ikiwemo zile za mipira ya kiume na kike kupitia bidhaa zao za DUME.
Tukio hilo limefanyika rasmi mapema jana Aprili 1.2016, ambapo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla alikuwa mgeni rasmi akiwakilisha Serikali katika tukio hilo kubwa na la kihistoria.
Akizungumza na wanahabari, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inapongeza juhudi za Taasisi za watu binafi ikiwemo T-MARC Tanzania wanavyofanya juhudi kubwa hapa nchini katika kuwafikia wananchi kupitia bidhaa zao hizo za kinga.
Dk. Kigwangalla amewapongeza kwa hatua hiyo tokea walipoanza hapa nchini kuanzia mradi hadi taasisi ambapo kwa hatua yao hiyo pia imesaidia na mapambano ya virusi vya UKIMWI kwani kupitia bidhaa zao hizo za kondomu kupitia kondomu za DUME zimekuwa msaada mkubwa sana kazi hizo wanazofanya wanaisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa sana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka alishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taassi hiyo kwani imeweza kutimiza malengo yake hapa nchini na itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega kwa kipindi chote.
Aidha, aliongeza kuwa, wataendelea kutoa huduma bora hiyo ya kinga kupitia bidhaa zao za mipira ya kinga yaani kondomu za DUME ilikuzuia mapambano ya virusi vya UKIMWI hapa nchini.
Awali Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua mabanda ya maonyesho ya miradi mbalimbali ya taasisi hiyo na kupata maelezo ya kwa kina kisha alipata wasaha wa kufungua rasmi jengo hilo la kisasa ambalo ni la ofisi za taasisi hiyo pamoja na kuzindua ghala maalum la kuhifadhia bidhaa hizo za DUME Condom.
Jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo hilo.


Ankal Michuzi,
ReplyDeleteHongera globu ya jamii kwa kuweka picha inayobeba taarifa ya uzinduzi yaani tumeliona jengo ktk picha halisi .
Maana siku za nyuma ilikuwa taarifa mfano uzinduzi wa bandari hatuioni picha ya bandari tunaona maandishi na picha nyingi za wanasiasa. Na kama picha ya bandari ina bahati basi itafichwa ''bonyezan hapa kwa picha zaidi''
Wasomaji wa globu ya jamii hu-''peruzii'' haraka haraka na hukatishwa tamaa wakiona taarifa imebeba picha zisizostahili kuwa kichwa cha habari husika . Maana sura za wanasiasa wengi zinajulikana.