Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Kikosi cha Maji, wakiwa katika boti, wakati wa zoezi la kutafuta miili ya watu waliozama baharini asubuhi ya leo, baada ya gari aina ya Toyota Hiace kuteleza kutoka kwenye Pantoni kabla ya kutumbikia na kuzama baharini. Imedaiwa kuwa gari hiyo ilikuwa na watu wawili, dereva mwanaume na abiria mwanamke. Waokoaji walifanikiwa kuopoa mwili wa dereva kwanza na baadaye wakaupata mwili wa mwingine mnamo majira ya saa tatu asubuhi ya leo. Mwanamke huyo inasemakana alikuwa anarejea nyumbani akitoka katika msiba wa ndugu yake uliotokea siku 9 zilizopita.
Mwili wa Mmoja wa watu hao ukitolewa mara baada ya kupatikana majini, juhudi za kuutafuta mwili zilifanikiwa masaa mawili badae.
 Zoezi la Upoaji likiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. LIES, LIES AND MORE LIES! Magari yakishaingia kwenye Kivuko iweje abiria wanabaki ndani? Sheria haziruhusu. Threre needs to be full accountability. Majipu hayo kama si wauaji.

    ReplyDelete
  2. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...