Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mstaafu, Harry Kitilya (kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania,  Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mastaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.

Aidha mpaka mtandao huu unatoka Mahakamani hapo Mawakili walikuwa bado wakihangaikia kupata dhamana baada ya kufutiwa shitaka hilo lililokuwa na kikwazo kikubwa cha dhamana.
Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. The mdudu, mimi naona umefika wakati wa kuharakisha ili tupate katiba mpya ambayo tutaanza nayo sifuli ili tuondokane na huu mfumo wa sasa wa mahakama zetu maana hakuna kitu kinachokera kuona mwizi wa kuku, simu, wapora mabegi wa dada zetu na Mama zetu, pamoja na vibaka kesi zao leo leo tena kwa haraka sana na wengi wao ndio waliokua kwenye magereza kama vile UKONGA, KEKO na SEGEREA na cha kushangaza hakuna hata mawakili wanao jitokeza kuwatetea au kuwapigania kwenye mambo ya zamana lakini tukija kwenye kesi za MAFISADI na WEZI wa Mali za umma hapo ndipo utapoona maajabu ya hii Tanzania yetu kwa kesi zao zinaenda mwendo wa KINYONGA huku MAWAKILI au watetezi pamoja na watu wa HAKI za KIBINAADAMU wanapigana vikumbo kwenye MAHAKAMA nchi nzima sasa watanzania wezangu tujiulize hivi wenye haki ni wenye kesi kubwa kubwa tuuuu? au vipi yaani mpaka machozi yananitoka poleni sana ndugu zangu wenye kesi ndogo ndogo

    ReplyDelete
  2. The Mdudu, leo umenena! Mawakili hao ni kama tai (ndege) au fisi. Wanaangalia kwa macho ya darubini, wapi kuna mzoga kau wananusa harufu ya mzoga wakiwa mbali; mara moja anakusanyika kula. Sio ajabu, huenda kuna collaboration na majaji ili kuwafungulia hao watuhumwa ili wagawane mapesa hayo ya bure waliyoibia umma!

    ReplyDelete
  3. Yani ndugu yangu mi nashangaa sana , Idara ya mahakama ni shida sana imejaa rushwa tu... hawa wakina kitilya ni wa kufungilia mbali wakafie gerezani.. wezi wakubwa hao...

    ReplyDelete
  4. Kalagabaho mwanakwetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...