Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanjaa (kushoto) alipowasili katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kuangalia mchezo kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makalla.Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union ya Tanga wakifanya mazoezi kabla ya kuanza mechi yao na Mbeya City jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union na Mbeya City wakisakata kabumbu jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifuatilia kwa makini mchezo wa mpira wa miguu kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jijini hapo. Kushoto kwa Mhe. Nnauye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makalla na wakwanza kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndg. Halhaji Kundya.Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia ushindi wa timu yao ya Mbeya City baada ya kuichapa timu ya Coastal Union ya Tanga mabao manne kwa sifuri jana katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...