Kwa mujibu wa imani na filosofia ya sanaa ya Yoga, Kufunga
ama kushinda Zaidi ya masaa 24 bila kula chakula ni moja ya mbinu adilifu
katika sanaa hii yenye mafunzo na tiba
asilia yenye zaidi ya karne moja.
Kufunga, kunywa maji na mbinu za mazoez yenye chimbko na mikao ya wanyama ni
misingi muhimu katika Sanaa hii ya mafunzo asilia ya mwanadam.
Katika somo la mafunzo ya Yoga, upo uthibiti wa
kuamini kwamba mwei mchanga na mwezi mpevu unaathari kubwa sana katika ubongo
wa mwanadamu kitabia na pia kimatendo. Ipo Imani kubwa sana kwa wana- Yoga au
“Yogi” kuamini kwamba mwili wa mwanadam uwejengwa na asilimia 70% ya maji.
Hivyo, kama jinsi mwezi unamvuto wa wimbi katika bahari ambayo husababisha maji
kutoweka ufukweni kwa muda kadhaa wakati wa mwezi mchanga na mwezi mpevu,
ndivyo hivyo jinsi mwili wa mwanadamu ambao unamaji asilimia 70% na kusababisha
wimbi kama hilo lenye athari kubwa kitabia na vitendo kwa watu wengi kipindi
hicho.
Kutokana na filosofia ya Yoga inaamini, siku tatu
kabla na siku tatu baada ya mwezi mchanga au mpevu, kunamvutano mkubwa wa wimbi
la maji mwilini kuvutwa katika ubongo wa
mwanadamambao usababisha athari kubwa kimawazo na hata kivitendo. Athari hiyo ni kama vile kutokuwa mtulivu,
hasira, uchokozi wa bila sababu, na pia tabia za ajabu ikiwemo hata ukatiri wa
vitendo. Katika kipndi hiki cha mwezi mpevu hutokea matukio mengi ya kinyama,
kama vile ghasia n ahata mauaji sababu wengi wa waathirika ushawishiwa kufanya
uovu kutokana na mvuto wa hilo wimbi na mwezi mpevu au mchanga.
Mwezi mchanga”Ekadashi” au mwezi mpevu “Purnima” katika lugha ya
“Sanskrit” ni moja ya siku muhimu sana katika folosofia ya Yoga kuhakikisha
unatuliza na kupoza fikra za mtu kupitia Sanaa hii ya kutafakari na kufunga kuimarisha
udhaifu wa athari ya mwezi katika ubongo wa mwanadam.
Mseomo ujulikanao “Lunar” ina fananishwa sana na
kile kiitwacho”Lunatic” ambao ni athari hizo zilizoelezewa hapo juu kuhuku
madhara ya mwezi mpevu au mchanga na jinsi unavyo sababisha ghasia katika fikra
na wengi kitabia.
Unapokuwa unafunga katika kipindi hicho cha siku
tatu kabla au tatu baadae, ni husababisha tumbo kavu kuvuta maji mwilini inayo
sababishwa na mwezi “Lunar”, na badala yake kuweza kumiliki hali ya usawa na uadilifu kitabia.
Hivyo tu kwa muktasari wa Sanaa ya Yoga, kufunga ni afya na muhimu sana kwa kuzingatia
ubora wa mawazo na maamzi ya busara katika kile kipindi kiitwacho “ Lunar”.
Baada ya kufunga masa 24, inashauriwa kisaa ya Yoga
kunywa angalau lita moja na nusu ya maji vuguvgu ya chumvi na ndizi iliyo wiva
sana kusafisha tumbo baada ya kufunga. Pia ni njia fasaha ya kutakasa utumbo
mkuu wa chakula mara moja kwa mwezi. Baada ya hapo, ndipo pale mafunzo ya
mazoezi ya yoga “Asanas” hufanya hali ya mwili kuwa imara na afya njema na
akili kuwa timamu pia.
Hii ni moja
ya kurasa za somo la Yoga na maisha kiujumla kutoka katika daftari la mwalimu
wa Yoga, Sensei Rumadha Fundi, mkufunzi wa Sanaa ya Yoga mwenye kushikilia
ngazi ya juu kabisa ya masomo hayo baada ya kuhitimu masomo Na Mchanga katika vyuo vya tawi hilo huko Sweden na
hatimaye kwa master wa Yoga “Guru, Shrii
Shrii AnandaMurtiji” huko Calcutta, India, 1987.
Sensei Rumadha Fundi katika zoezi la Yoga. Chini ni binti yake ambaye naye anafuata nyayo za baba yake kwenye mazoezi
Fred Macha hapo kimyaaaaaaaa!!!! mwenyewe Sensei Rumadha mtoto wa kitovu jiji Karikoo akichambua kwa undani masuala ya Yoga,Big Up Sensei Rumadha
ReplyDelete