Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na kuona namna ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS, mkoani kigoma Eng. Narcis Choma (wa tatu kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), barabara ya Simbo-Kalya yenye urefu wa zaidi ya Km 200 Kusini mwa Ziwa Tanganyika itakayoanza kujengwa hivi karibuni wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wananchi wa Ilagala, Sunuka, Karago, Herembe, Kapalamsenga, Mgambazi, Lukoma hadi Kashagulu ya namna sahihi ya kutumia kivuko cha MV. Malagarasi, mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akioneshwa namna ya huduma za uongozaji ndege zianvyofanyika katika kituo cha Kigoma. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole na katikati ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe akifatilia.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...