Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu
Mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri
wasiokuwa na Wizara Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya
Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na
Serikali pamoja na wananchi kadhaa ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman
Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.
Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Mhe. Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla
Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja
na viongozi wa vikosi vya Ulinzi.
Walioapishwa katika hafla hiyo ni Waziri,
Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman. Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya Mhe.
Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe
Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto
Mhe. Moudline Castico.
Wengine
ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa
Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid A. Karume. Waziri wa
Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed. Waziri wa
Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma na Waziri wa Ardhi,
Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama Aboud Talib.
Kwa
upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis Juma Maalim. Naibu Waziri wa Afya
Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe.
Mmanga Mjengo Mjawiri.
Wengine
ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahmed
Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo nan Uvuvi Mhe. Lulu Msham
Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Bibi Choum
Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma
Makungu Juma.
Aidha, Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa
Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said
Soud Said kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara
Maalum pamoja na Mhe. Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri
Asiekuwa na Wizara Maalum.
Kwa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42,
43,44 na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ameunda Wizara 13
za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri
wa Wizara hizo pamoja na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa
Baraza la Mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu
Nafikiria tu: Hivi ingekuwaje kama Rais Magufuli angekwenda kufanya kazi Zanzibar kama Rais kwa kuda mfupi? Maana naona kama huku bara kuna mabadiliko, mambo ya majipu,nk lakini kule ni kama mambo ni yale yale tu. Just thinking!
ReplyDeleteMdau wa mwanzo hapo juu you're right. Kule nako kungepata mkamuwaji khasa, kile kisiwa ni kidogo sana mara moja kingeweza kubadilika kimaendeleo, kiusalama wa wananchi na mali zao, kiafya na mazingira kwa jumla na yote yakhusuyo uchumi na kijamii kwa jumla. Labda bado mapema mno kulitabiri hilo, time will tell, ngoja tuvute subira.
ReplyDelete