Na kitengo cha Sheria
na Mahusiano,
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
TIMU ya Uchukuzi Sports Club imepania kufanya vyema
kwenye mashindano ya Sikukuu ya
Wafanyakazi (Mei Mosi) yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 16 mwaka
huu.
Mwenyekiti wa timu hiyo inayoundwa na wafanyakazi wa
taasisi zinazounda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mohamed Ally
alisema kuwa timu yake itafanya vizuri katika mashindano hayo, kutokana na
maandalizi kabambe waliyofanya.
Ally alisema kuwa kwa sasa wako katika mazoezi
makali kujiandaa na mashindano hayo, ambayo yatafikia kilele siku ya Mei Mosi
mjini Dodoma.
Ally alisema Uchukuzi Sports Club inaundwa na timu
za michezo ya soka, netiboli, kuvuta kamba, bao, karata, riadha, baiskeli na
vishale.
Alisema kuwa wana uhakika timu yao kufanya vizuri
katika mashindano hayo, kutokana na kufanya mazoezi kwa muda mrefu chini ya
makocha wazoefu wa michezo hiyo.
Ally aliwataja baadhi ya makocha hao kwa upande wa
soka kuwa ni pamoja na Kenny Mwaisabula, Robert Damian, Terry, Kingsley Malwilo
na Abunu Issa, ambao wameifanya timu yao kuwa tishio kwa timu zingine, wakati
netiboli inafundishwa na mchezaji mkongwe Judith Ilunda.
Alisema kuwa timu zao hizo zimekuwa zikicheza mechi za
kirafiki na timu mbalimbali, ili kuwawezesha makocha kubaini makosa na kufanya
marekebisho ya mwisho kabla timu hiyo haijaondoka kwenda Dodoma.
Naye Meneja wa Uchukuzi Sports Club, Robert Damiani
alisema kuwa timu yao inatarajia kwenda Dodoma Aprili 14 tayari kwa mashindano
hayo.
Damiani alisema wanauhakika wa kufanya vizuri na
kuvunja rekodi ya mwaka jana ya kutwaa vikombe 13, kati ya hivyo vitano vikiwa
ni vya ushindi wa kwanza, wakati vilivyosalia walishika nafasi ya pili na tatu.
Timu
ya soka ya Uchukuzi Sports Club iliyopo chini ya Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na
Mawasiliano ikifanya mazoezi wakijiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi
Makipa wakila tizi maalumu
Kikosi
kabambe cha timu ya soka ya Uchukuzi kikiwa pamoja na kocha na meneja wa timu
hiyo Robert Damiani (kushoto).
Wachezaji wa
timu ya wanawake ya kuvuta kamba ikiwa kwenye mazoezi katika viwanja vya JNIA.
Kikosi kabambe cha wanawake cha klabu ya Uchukuzi wakifanya mazoezi
kabla ya kuvuta kamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...