Na
Afisa habari RS MWANZA.
Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella (pichani) ametoa saa 24 kwa
kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi
kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba
kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)
Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha
kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha
kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya
komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.
“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00
mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema
Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo
kompyuta hiyo.
Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri, kaimu
mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo, alidai kupokea taarifa za kupotea kwa
Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri
ya Ukerewe akimuelezea upotevu huo.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe,,
kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa
muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi
kwa mazoea.
”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote
waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka
ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema
Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye
kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.
Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe
Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni
shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya
imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi
katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.
Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara
yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea
wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe
inakuwa wilaya ya saba huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye
halmashauri za Buchosa na Sengerema yenyewe.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...