Wakala wa Nishati Vijijini REA, wametoa msaada wa taa za kutumia mionzi ya jua katka kijiji cha Kisanga kitongoji cha Kiala; Wilaya ya Iringa Kitongoji hiki ni kile kilichokumbwa na mafuriko na kaya zaidi ya 100 kukosa mahala pa kuishi. Kijiji kiliamua kuwatengea eneo ambalo watajenga makazi mapya. Akitoa msaada huo Bi Jaina Msuya Afisa habari REA aliwaasa wananchi kutunza taa hizo na kuhakikisha zinachukua muda mrefu. Akipokea msaada huo Mkuu wa wilaya Iringa bwana Richard Kasesela alisema taa hizo zitasaidia kupunguza kutoa mwanga pia watoto wanaweza kujisomea usiku na hatari ya nyoka itapungua. REA wametoa taa zenye thamani ya tsh Mil 7. Wananchi wa kitongoji hicho wanaendelea na shughuli za ufyatuaji matofali ili kujenga nyumba.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akitoa msaada wa taa za kutumia mionzi ya jua katka kijiji cha Kisanga kitongoji cha Kiala; Wilaya ya Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akikabidhi misaada hiyo toka REA kwa waathirika wa mafuriko Kijiji cha Kisanga Iringa
Bi Jaina Msuya Afisa habari REA akiwaasa wananchi kutunza taa hizo na kuhakikisha zinachukua muda mrefu kwa waathirika wa mafuriko Kijiji cha Kisanga Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akishudiwa na Bi Jaina Msuya Afisa habari REA akionesha wananchi namna ya kutunza taa hizo na kuhakikisha zinachukua muda mrefu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...