Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu JANUARY
CLAUDIO KISANKO tunatoa shukrani za dhati kwa wote walioshirikiana nasi kwa
hali na mali katika kipindi kigumu cha kumuuguza mpendwa wetu hadi alipoitwa na
Mungu tarehe 21 Machi 2016 katika Hospitali ya TMJ na kupumzishwa katika nyumba
yake ya milele tarehe 28 Machi 2016 katika makaburi ya Kinondoni.
Kwa heshima kubwa tunatoa shukrani za dhati kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Ndugu, Majirani wa Kinyerezi na Ubungo, Marafiki, Wanajumuiya wa Mt. Anna mama wa Bikira Maria na kanda ya Mt. Augustino wa Hippo Kinyererezi na wale wote wenye mapenzi mema kwa sala na dua zenu katika kipindi hiki kigumu.
Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari na wauguzi wote wa Hospitali ya TMJ chini ya uongozi wa Daktari Kapiteni Lusangulira akishirikiana na Daktari Kaduri na Azzah.
Aidha tunamshukuru Baba Paroko Fr. Evarist wa Kanisa Katoliki la Mt. Boniventure la Kinyerezi kwa kumpatia huduma za kiroho marehemu ikiwa ni pamoja na mpako wa wagonjwa na kisha kuendesha Ibada ya mazishi.
Kwa vile si rahisi kuwataja wote, tunaomba mpokee
shukrani zetu za dhati kwa moyo wa Upendo kwa familia hii.
Misa ya Shukrani itafayika siku ya Jumamosi tarehe
30 Aprili 2016 katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Boniventure, Kinyerezi saa
3:00 asubuhi. Familia inawakaribisha wote siku hiyo kanisani na baadae saa 6:00
kwenye chakula cha mchana nyumbani kwa marehemu Kinyerezi
BWANA AMETOA
NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE (Ayubu 1:21)
Raha ya
Milele umpe ee Bwana, Na Mwanga wa Milele umwangazie,
Apumzike kwa
Amani.
AMINA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...