Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari jijini Arusha (hawapo pichani) kuhusiana na Kampeni ya siku Kumi ya Usafi wa Mlima Kilimanjaro inayotarajiwa kuanza kesho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania, Cyril Ako.
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kesho tarehe 21.04.2016 litazindua Kampeni Maalum ya
siku 10 ya usafi wa Mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo Utafanywa na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Mhe. Said Mecky Sadik.
Kazi hii ya kusafisha Mlima Kilimanjaro itafanywa na watumishi wa hifadhi kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali wa utalii zaidi ya 200, wakiwemo mawakala wa utalii (tour operators),
waongoza wageni (guides), wapagazi (porters) na wapishi (cooks) wanaowahudumia watalii
katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.
Usafi huu utahusisha maeneo mbalimbali ya hifadhi kama vile njia za kupandia mlimani, maeneo
ya kupiga kambi, maeneo ya mabanda, na maeneo ya kupumzikia wageni (picnic sites).
Kampeni hii ni muendelezo wa utaratibu wa kawaida wa hifadhi unaofanyika kila wakati
kuhakikisha maeneo ya hifadhi hasa yanayotumika na wageni yanakuwa katika viwango vya
kimataifa vya utoaji huduma kwa wageni. Huu ni utaratibu wenye lengo la kuwahamasisha
wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wanauweka Mlima Kilimanjaro katika hali ya usafi muda
wote.
Mlima Kilimanjaro unachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 60 ambazo ni sawa na asilimia 34 kwa
mwaka katika mapato ya TANAPA. Aidha, Mlima Kilimanjaro hutoa ajira zaidi ya laki
tatu(300,000) kwa mwaka kwa Watanzania wanaofanya shughuli za utalii mlimani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...