Kuz: 27.01.1943 – Kuf: 28.03.2016
Familia ya Bw. Stephen Philiph Assey wa Kijitonyama Dar es Salaam, inayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba, mazishi na hatimaye matanga ya Mama/Bibi yao mpendwa, Theresia.S.Assey, aliyefariki dunia alfajiri ya Jumatatu ya 27th March, Kijitonyama Dar es Salaam na kuzikwa Makaburi ya Kinondoni, Alhamisi ya 30th march , 2016.
Kwa vile waliwotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za jumla ikiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu.
Mmeonesha upendo wa kweli kweli kwetu kama Familia na kwa Mama/Bibi yetu Theresia ambaye angerejea kwenye uzima tena, naye bila shaka yoyote angetoa shukrani za dhati ya moyo wake.
Hata hivyo, tunapenda kutoa shukurani kwa makundi machache ya marafiki ambao mchango wao utabakia kwenye nyoyo za wazazi na familia yetu tukianza na majirani na marafiki wa karibu wa Familia walioko Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Mbeya na kwingineko na nje ya Afrika Mashariki, ambao michango yao kamwe haitasahaulika.
Familia pia inapenda kushukuru Kanisa Katoliki la Mwananyamala chini ya Paroko wake na wanajumuia ya Mtakatifu Clara Mtaa wa Makumbusho Dar Es Salaam, Uongozi na Washarika wa Biblical Counselling and Intercession Centre(BCIC)-Mbezi Beach. kwa huduma kubwa za kiroho wakati wa msiba huo mkubwa uliotufika.
Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Madaktari, na kwa Wauguzi na wa Hospitali za Kairuki, Regency hospital, Abass medical clinic na Muhimbili Dar es Salaam kwa juhudi zao za dhati za kutaka kuokoa maisha ya Mama yetu.
Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa,Mahakama ya Tanzania Airtel-Nokia, Wafanyakazi wa Chuo kikuu Cha Ardhi, NMB-Mbezi Branch na CRDB Bank kwa michango yenu, ilitufariji na tutaendelea kukumbuka ukarimu wenu daima.
Mwisho Tunawashukuru nyote mlioweza kufika nyumbani Kijitonyama na Makaburini Kinondoni kumhifadhi Bibi Tere. Hatuna cha kuwalipa, Mungu atawalipa.
“Mathayo 5:8:-Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Bwana”
Mungu awabariki sana



Rest in eternal peace mom...
ReplyDeleteRest in eternal peace mom..will always love u
ReplyDeleteRest in eternal Peace mom...we will always have u in our hearts.
ReplyDeleterest in peace granny
ReplyDelete