Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetia saini ya makubaliano maalum (MoU)
na Sekretarieti ya AMCOW ya kukubali Tanzania kuwa mwenyeji wa
Mkutano Mkuu wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW)
na Maadhimisho ya 6 ya Wiki ya Maji ya Afrika.
Makubaliano hayo yalisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Inj. Mbogo Futakamba na Mtendaji Mkuu wa AMCOW, Bai
Mass Taal leo mchana, katika Mkutano na Waandishi wa Habari
uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo, Ubungo Maji.
Mkutano huo na Maadhimisho hayo ya Kimataifa yatafanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
kuanzia tarehe 18-22, Julai na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Inj. Mbogo
Futakamba akizungumza, kushoto ni Mtendaji Mkuu wa AMCOW,
Bai Mass Taal na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji,
Dkt. George Lugomela.
Mtendaji Mkuu wa AMCOW, Bai Mass Taal akizungumza, pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Inj. Mbogo
Futakamba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Inj. Mbogo
Futakamba na Mtendaji Mkuu wa AMCOW, Bai Mass Taal wakisaini
hati za makubaliano huku wakishuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa
Rasilimali za Maji, Dkt. George Lugomela.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...