Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya NMB, Richard Mwalwiba amekabidhi rasmi vikombe vya ushindi wa Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker ikiwa ni pamoja na kutoa shukrani kwa uongozi wa benki hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu yake. Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, ambapo uongozi wa timu ya mpira wa miguu ya NMB ilipofanya mazungumzo na uongozi wa Benki ya NMB kuelezea mafanikio na changamoto za mashindao hayo. Timu ya NMB ilifanikiwa kutwaa vikombe viwili katika ligi ya ‘Brazuka Kibenki’ iliyoshirikisha mabenki mbalimbali nchini Tanzania. NMB ilifanikiwa kutwaa kombe la ushindi wa tatu wa mashindano hayo pamoja na Kikombe cha Timu Bora iliyojipanga vizuri katika ushiriki wa mashindano hayo. 
 Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa NMB , Bi. Ineke Bussemaker kabla ya kumkabidhi vikombe walivyojishindia katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ iliyomalizika hivi karibuni. Kulia ni Meneja wa Timu ya NMB, Bi. Josephine Kulwa pamoja na mchezaji wa NMB aliyechaguliwa kuunda kikosi cha timu ya mabenki  Hezbon Mpate(katikati.Kwa upande wake Meneja wa Timu ya NMB, Bi. Josephine Kulwa alisema ili kujiweka vizuri katika mashindano yajayo tayari wachezaji wote wa NMB wameanza mazoezi ya aina mbalimbali chini ya wakufunzi wa mazoezi. “Sisi tupo fiti muda wote kimichezo, tunavyozungumza hivi sasa tayari wachezaji wanafanya mazoezi yote ya  kujiweka vizuri zaidi,” alisema Bi. Kulwa.

 Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker moja ya vikombe walivyoshinda
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea vikombe  vya ushindi kutoka kwa viongozi wa timu ya NMB

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...