Mkurugenzi huduma na elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo (Kushoto) akizumgumza na waandishi wa habari (hapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana kukusanya mapato kupitia tasinia ya mziki na filamu kwa kuhakikisha bidhaa za filamu na mziki zenye stemu za kodi ndizo zinazoingizwa sokoni ili kulinda kazui za wasanii wa hapa nchini.
Katibu Mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandisho wa ha bari jijini Dar es Salaam leo, amewaomba wadau wa sanaa na wote wanaosambaza na kuuza kazi za Filamu na Mziki hapa nchini ambazo hazijabandikwa stempu halali za kodi kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata stempu hizo katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ili wawe halali kuuza bidhaa hizo.
anayefuata ni Mkurugenzi huduma na elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imefungia maduka ambayo yalikuwa yakiuza kanda za muziki na Filamu bila kulipa kodi pamoja na kukosesha msanii kupata haki yake kutokana na kazi zao.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo amesema katika operesheni walioifanya hivi karibuni kwa kushirikiana na kampuni ya Majembe wameweza kukamata CD na DVD ambazo hazina stempu za kodi na kusababisha wasanii kukosa haki yao kwa kazi walizotweta jasho.
Amesema katika operesheni hiyo wameweza kukamata CD na DVD za nje zinazoingizwa nchini ambazo,zimekuwa zikilalamikiwa kwa kusababisha kazi za ndani kukosa soko.
Kayombo amesema katika operesheni hiyo wameweza kukamata CD na DVD 656,579 zenye thamani zaidi ya sh.bilioni moja ambazo zilikuwa zikisambazwa bila kufuata taratibu na sheria na kati ya hizo 650,101 ni za kutoka nje ya nchi huku kazi ndani zikiwa 6,478 ikiwa na kodi iliyokadriwa ni zaidi ya sh.milioni 31 na gharama za stempu ni zaidi ya sh. Milioni 11.
Maduka waliouafungia ni kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano kwa TRA kufanya kazi yake ya kutafuta kodi ambayo ni Kilimanjaro House Music, 1 Shop near Kilimanjaro Music, Siku Hazifanani DVD Move, Lum Mult Technology & General Supplies ,Fetty Big Star maduka hayo yanapatikana Kariakoo, GM Video Centre Banana Ukonga pamoja na Unknown Mbagala.
Amesema katika operesheni hiyo wameweza kukakamata mitambo 47 ya kudurufu kazi za wasanii CD na DVD, Komputa nne na UPS moja na wafanyabiashara wenye mitambo hiyo ni, Peter Zakaria Mkude mkazi (Mabibo), Ismail Seif (kigogo), Auguster Company (Kariakoo), Hillary Proches (Sinza),Babu Juma Kundawi (Mwanayamala), Ignus Peter Mushi (Mwananyamala).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...