Kikosi cha Uchukuzi SC kabla ya mechi na Ukaguzi.
 Mchezaji wa timu ya Uchukuzi SC, Abubakar Mwamachi (mwenye namba 22 mgongoni) akifunga kwa kichwa bao la kwanza. Uchukuzi iliishinda Ukaguzi kwa magoli 3-1.
 Mkuu wa benchi la ufundi la timu ya soka ya  Uchukuzi SC, Kenneth Mwaisabula (kulia) akiongea na mmoja wa wachezaji wa timu ya Ukaguzi, mara baada ya mchezo wao kumalizika. Uchukuzi walishinda kwa magoli 3-1.
TIMU ya soka ya Uchukuzi SC imeng’ara kwa kuifunga Ukaguzi mabao 3-1 katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Uchukuzi SC ambayo chini ya benchi la ufundi mahiri linaloongozwa na Kenneth Mwaisabula ‘Mzazi’ ambaye ni Mkuu wa benchi hilo,  huku Elutery Muholeli ni kocha na Robert Damian ni meneja wa timu hiyo, waliwapeleka puta wapinzani wao na kuandika bao la kwanza lililofungwa kwa kichwa na Kado Nyoni, baada ya kuwahi mpira wa kona safi iliyochongwa na Omar Said ‘Chidi’ katika dakika ya 34.
Hatahivyo, Ukaguzi walisawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Ben Chezue aliyepiga mpira wa adhabu ndogo uliokwenda moja kwa moja golini. Chezue aliingia dakika 49 kuchukua nafasi  ya Deo Masanja aliyekuwa ameumia.
Uchukuzi SC iliongeza bao katika dakika ya 72 lililofungwa Issac Ibrahim aliyeachia shuti kali, lililomshinda kipa wa Ukaguzi, Shomari Dumba.
Nahodha wa Uchukuzi SC, Francis Charles alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu katika dakika ya 90 kwa njia ya penati baada ya Bilal Mleli kushika mpira katika eneo la hatari.
Uchukuzi SC iliyokuwa ikicheza kwa kuonana, awali timu Uchukuzi SC ilikosa magoli kibao ya wazi, baada ya wachezaji wake Abubakar Mwamonchi katika dakika ya 25 kupiga mpira uliopita pembeni kidogo ya goli, huku Francis alishindwa kuunganisha krosi ya Masoud Juma katika dakika ya 30, tena Francis aliyeisumbua ngome ya Ukaguzi katika dakika ya 58 alipaisha mpira akiwa karibu na kipa.
Akizungumza mara baada ya mechi, kocha Muholeli alisema Ukaguzi ni moja ya timu ngumu, lakini aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kutoka na ushindi mnono, ambao umesaidia kusafisha njia.
“Hapa tumekuja kushindana na kila mechi kwetu tunaiita ni fainali, hivyo timu zote zilizokuja hapa ni nzuri, ila tunataka tushinde mechi zote ili tujiweke pazuri kushinda na kutwaa kombe hili, kwani tumeshafika fainali mara nne,” alisema Muholeli.
Naye Mwenyekiti wa Uchukuzi SC, Mohamed Ally alisema wamekuja Dodoma kuchukua ubingwa na anauhakika wa timu yake itafanya vyema kutokana na nidhamu ya mazoezi wanayofanya kila.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...