MKURUGENZI wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Rashid Salum pamona na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Hatibu Chaulembo wamelazimika kutoka nje ya kikao cha baraza la madiwani baada ya uongozi wa chama cha walimu (CWT) wilayani humo kuvamia katika kikao hicho kwa lengo la kwenda kulalamikia madai yao ikiwemo malimbikizo ya mishahara yao.
Walimu hao wa shule za msingi na sekondari wakiongozwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Rufiji walifunga safari ya kwenda katika ofisi ya Mkurugenzi huyo lakini waliambiwa yupo kikaoni ndipo walipoamua kuandamana mpaka kwenye ukumbi huo wa mikutano na ndipo walipomwandikia ujumbe wa kutaka kuonana nae ili watoe kilio chao.
Wakizungumza kwa uchungu mara baada ya Mkurugenzi na Mwenyekiti kuamua kukubali na kuamua kuacha kuendesha kikao na kutoka nje ya ukumbi huo wa mikutano, Mwenyekiti wa CWT Hamza Marwile pamona na Katibu wake Antony Mangwary ndipo walipoamua kutoa malalamiko yao ya malimbikizo ya madai yao mbele ya viongozi hao wa halmashauri katika kikao cha dharura kilichofanyika chini ya mti huku mvua ikiendelea kunyesha.
Mwenyekiti wa CWT Hamza Marwile alisema kwamba wameamua kufunga safari zaidi ya kilimota 75 kwa ajili ya kwenda katika ofisi za mkurugenzi kwa ajili ya kutoa kilio chao kwa muda mrefu kutokana na walimu walimu wa Wilaya hiyo kunyanyasika kutokana na kutopata haki zao za msingi.
Marwile alisema katika siku za nyuma walikuwa wanapeleka malalamiko ya madai yao kwa mwajiri wao ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji lakini cha kushangaza madai hayo bado yalionekana kutofanyiwa utekelezaji wa haraka ndio maanda wakaamua kufunga safari ya kwenda kuonana na wahusika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...