Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela amefunga mafunzo ya "Kungfu" yaliyokuwa yanaendeshwa na SHOKINJI KEMPO. Washiriki kutoka Dares salaam na Dodoma walionyeshana ufundi wa kung Fu na wengine walipandishwa madaraja. katiba hotuba yake aliwaomba Kemp hiyo kuwa walinzi wa amani kwani sifa kubwa ya wacheza kungfu ni kuhakikisha amani. Mwanzilishi wa Shokinji Kemp alifariki tarehe 14 mwezi wa 5 miaka 60 iliyopita huko Japan.
Mwenyeji wa mashindano hayo Diwani wa Kitanzini ambaye yupo daraja la juu (Mkanda mweusi) alishukuru sana uwepo wa Mkuu wa wilaya na kuahidi kumsadia katika kulete amani na utulivu pamoja na kuzuia vijana kuingia kwenye tabia mbaya za uvutaji bangi na ulevi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa zawadi ya mpira kwa mwakilishi wa kituo cha watoto taima cha Korongoni kwenye hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa na wanamichezo wa Kungufu wenye mikanda myeusi na Kijani kwenye hafla hiyo
washiriki watoto wakionyesha umahili wao wa kungfu
Diwani kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa (kulia) akionyesha umahili wake wa Kung fu.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...