Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limerudisha nyuma tarehe ya mechi ya fainali kati ya Yanga na Azam ambapo awali ulitakiwa kufanyika Juni 11.

Mechi hiyo sasa inatarajiwa kufanyika wiki ijayo Mei 25.

Akizungumza kwa niaba ya TFF, Afisa habari Alfred Lucas amesema kuwa mechi hiyo itafanyika Jumatano ijayo badala ya tarehe ya awali iliyokuwa imetajwa na Shirikisho hilo.

Amesema kutokana na kumalizika kwa ligi Mei 21 na timu zitakuwa zimekaa muda mrefu zikiwa hazina mechi zozote.

"Ligi kuu inamalizika Jumamosi Mei 21 na wachezaji watakaa muda mrefu bila kuwa na mechi kwahiyo tumeonelea kuwa turudishe nyuma kutoka Juni 11 mpaka Mei 25,"amesema Lucas.

Kufuatia kurudishwa nyuma kwa mechi hiyo ambayo ndiyo inatoa muwakilishi wa Michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, TFF imezitaka timu hizo kujiandaa kwani zitakuwa  zimemaliza mechi zao za ligi kuu.

Yanga watamaliza mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Majimaji mkoani Songea huku Azam watakuwa Chamazi kuumana Mgambo JKT.

"TFF imezitaka Yanga na Azam kujiandaa zaidi  bado watakuwa hawajavunja kambi kwani wanamaliza ligi Jumamosi ya wiki hii,"amesema Lucas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2016

    Ubabaishaji tu...yaani manabadilisha ratiba hovyo hovyo tu. Hamkuliona hilo toka mwanzo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...