Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .
ALIYEKUWA Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan ameinyofoa kesi yake ya uchaguzi mahakamani aliyokuwa ameifungua ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Mbunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Azzan amesema kuwa kuondoa kwa kesi hiyo ni kutaka kujipa muda wa kufanya shughuli zake na Mbunge wa Kinondoni aendelee kuhudumia wananchi wa Kinondoni kutokana na watu nia ni kuwatumikia wananchi.
Uamuzi huo umetolewa leo na Azzan kupitia mwanasheria wake mbele Jaji wa Mahakama Kuu ya Mbeya, Jaji Chochi ambapo mahakama ilikubali maamuzi hayo yaliyolewa na upande wa mashitaka.
Naye Wakili wa Mbunge wa Kinondoni, Juma Nassoro amesema kuwa walikuwa wamejipanga kuhakikisha kesi hiyo wanashinda lakini kutokana na Azzan kuomba kuiondoa kesi hiyo,basi Mbunge Mtulia aendelee kuwahudumia wananchi.
Nae Mbunge wa Jimbo hilo, Mtulia amesema kuwa ametumia muda mwingi kuja kusikiliza kesi na kushindwa kuchangia katika bunge la bajeti linaloendelea baadhi ya wizara.
Amesema sasa atahudumia wananchi wake vizuri kutokana na muda atautumia ofisini ikiwa ni pamoja na ushiriki katika bunge kuwakilisha wanakindoni katika matatizo yanayo wakabili.
Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akimpongeza Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia kufuatia kuiondoa kesi yake ya
uchaguzi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mbunge huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini
Dar es Salaam.

Mbunge
wa Kinondoni, Maulid Mtulia akiingia mahakamani katika kesi ya
uchaguzi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Idd Azzan leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini
Dar es Salaam.

Aliyekuwa
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akiingia mahakamani, ambapo alifungua
kesi ya uchaguzi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CUF,
Maulidi Mtulia leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar
es Salaam.

Baadhi ya watu waliofika kuisikiliza kesi hiyo.Picha na Emmanuel Massaka-Globu ya Jamii.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...