Na Shamimu Nyaki WHUSM

 Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa  Utamaduni Duniani Serikali imeitaka jamii kuhifadhi kulinda na kuheshimu utamaduni wa nchi kwa vile ndio kitambulisho cha Taifa letu ili kuweza kutambulika ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,utamadunu,Sanaa na Michezo  Bi.Lily Beleko wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa  Utamaduni Duniani ambapo kauli mbiu ya madhimisho ya mwaka huu ni” Utamaduni wa Uadilifu na Nidhamu ya Kazi Huleta Maendeleo”, “Sasa Kazi  Tu”
.
Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni Bi.Lily Beleko amesema kuwa ni wajibu kwa kila  mtanzania kuheshimu  Utamaduni wetu na kushiriki kikamilifu katika  kuutambua, kuujenga, kuuendeleza  na kuurithisha kwa vizazi vingine.“Siku hii ni maalumu kwa kila mtanzaniana na kila mmoja hana budi kukubaliana na harakati hizi za kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni wetu kwa ajili ya vizazi vijavyo”Alisema Bi Lily. 

Bi.Lily Beleko ameongeza kuwa  nchi haiwezi kutambulika na kuheshimika  kama Taifa huru bila kuwa na Utamaduni wake hivyo kuwepo kwa maadhimisho haya kunaipatia jamii fursa ya kuendelea kukumbushana ,kuhamasishana na kuhimizana katika kuuenzi utamaduni wa nchi.

Siku ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 Mei, ambapo siku hiyo imeteuliwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuona umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni na hivyo kupitisha Azimio Na 57/249 mnamo mwaka 2002.
 Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni yanayotarajia kufanyika  Mei 21 mwaka huu ,kulia ni Afisa Habari  wa Wizara hiyo Bw.Benjamini Sawe.
 Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa habari  (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni yanayotarajia kufanyika  Mei 21 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...