KAMPUNI ya Peri hapa nchini inayojihusiaha tecknolojiia ya ujenzi hapa imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini, Issack Peter.
Kampuni ya Peri ni ya nchini Ujerumani yenye makao makuu yake maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam
kampuni hiyo inaweza kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na teknolojia wanayoitumia katika ujenzi wa Majengo marefu mbalimbali kuwa katika teknolojia yao haitumii mti kwaajili ya ujenzi.
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini (NHC), Issack Peter (katikati) Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser (Kushoto) na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Peri, Giuseppe Rosiello wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampuni ya Peri hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini, Issack Peter akizungumza katika uzinduzi wa Kampuni ya Kijerumaji hapa nchini ya Peri jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Shirika la nyumba hapa nchini lipo katika mpango wa kuendeleza nyumba 6000 hapa nchini kwaajili ya makazi na Biashara na nyumba hizo zipo za Gharama nafuu, gharama za kati pamoja na gharama za juu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser akizungumza katika ufunguzi wa kampuni ya Peri jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kampuni ya Peri ni kampuni inayo saidia katika kupunguza uharibifu wa mazingira hasa kupunguza ukataji wa miti pia inaendeleza majengo mbalimbali.





Teknolojia zipo aina mbalimbai zikiwepo za polystyrene panels na za aina nyingine nyingi zinazoweza kutumika kuboresha makazi ya wananchi hasa hasa nyumba za gharama nafuu za vijijini. Ndiyo maana katika mpango wowote utakaotarajiwa kuboresha makazi ya wananchi tuwe na ufahamu mzuri nyumba za aina gani zinafaa mahali gani. Kwa sababu siyo kote kutahitaji matofali ya kuchoma ili kulinda misitu, kwingine kutahitaji matofali ya Block (Brick and Mortar) lakini kwingine hata Panels zinazotokana na technology ya ujenzi wa kisasa zina bei nzuri zinazoweza kushusha gharama za ujenzi. Ndiyo maana chuo kikuu kama cha Ardhi kwa mfano katika utafiti wake kinatakiwa siyo tu kituchoree ramani zenye nyumba bora za kisasa zikiwa na huduma zote bali kushauri sehemu zipi zinahitaji kuboresha nyumba kwa kutumia teknolojia gani. Wanafunzi wao wanaweza kuja kufanya field ya kutengneza au kutumia wanahitimu walio vijijini kuzishughuikia. Tukiwa na mipango mizuri ya maendeleo itatatua pia issue ya kuhusisha vijana wanaotafuta ajira huko waliko ikiwemo vijijini.
ReplyDeleteTakwimu za sensa iliyopita zilionyesha nyumba bora nchini kuwa asilimia 43 hatua za makusudi zifanyike kuongeza asilimia hiyo hasa vijijini kufikia 75 au zaidi katika miaka mitano ijayo.
ReplyDelete