Rais wa Simba Evance Aveva akifafanua jambo
NA Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Simba umelaani vikali kitendo cha Hassan Kessy na Ibrahim Ajib kufanya vitendo nje ya mkataba wao na kusema ni usaliti kwa klabu hiyo.









Kessy (kulia) alisimamishwa na uongozi wa Simba baada ya kukutwa na kosa la kufanya madhambi kwa makusudi na kupelekewa kupatiwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Toto uliomalizika kwa Simba kupoteza mechi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Simba Evance Aveva amesema kuwa kitendo cha Kessy kusaini katika klabu nyingine akiwa bado ana mkataba na Simba kinaonekana ni kitendo cha kihuni na kinachothibitisha kuwa amekuwa anahujumu timu.
Ajibu  (kulia) naye amefanya kosa lililopelekea kupata kadi nyekundu na usiku huo huo majira ya saa 3 usiku anapiga simu na kusema kuwa amepata timu anakwenda kufanya majaribio nchini Afrika kusini amesema  Aveva.
"Hawa wachezaji wawili wameonyesha ni wamekuwa wanahujumu timu na tumeona makosa wanayoyafanya ni ya wazi kabisa,"amesema Aveva.
Aveva amesema kessy amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu lakini ameshasaini kwa wapinzani wetu na tumeliona hilo na ligi ikiwa bado haijaisha na ushahidi upo kutokana na matendo yake yote aliyokuwa anayafanya.
Kwa upande wa Ajib, kamati ya maadili itaangalia namna gani watamuadhibu kulingana na kitendo cha kufanya kosa na kisha kuaga kwenda nchini Afrika kusini.
Wakati huohuo, klabu ya Simba inafanya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa mchezaji wao Patrick Mutesa Mafisango aliyefariki Mei 17 2012 kwa ajali ya gari.
Mafisango (kushoto) alifariki mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu iliyoishia kwa Simba kuwa mabingwa huku akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli na katika ligi pamoja na kufunga goli la mwisho.
Akitoa salamu hizo za maombolezo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema kuwa bado watakuwa na kumbukumbu hiyo daima kwani Mafisango alikuwa ni moja ya wachezaji  waliokuwa na kipaji kikubwa sana."Daima tutaendelea kumkumbuka sana kwani ni moja ya wachezaji wenye kumbukumbu kubwa sana katika klabu yetu ya Simba na mpira kwa ujumla,"amesema Manara
Manara amesema kuwa wataendelea na utaratibu wao wa kumuombea kila mwaka ikiwa ni moja ya kumbukumbu yao muhimu, Baada ya kufariki kwa Mafisango, Klabu ya Simba waliamua kuweka heshima kwa kutokuitumia tena jezi namba 30 ambayo ilikuwa inavaliwa na mchezaji huyo mwenye asili ya Kongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...