Hivi jamani baadhi yetu tutabadilika lini? Kwa nini hatutaki kuyaelewa ama kuyakubali mabadiliko ya kimazingira. Wewe umeambiwa hiyo ni barabara maalum ya magari ya mwendo kasi lakini bado kutokana utashi wako unaoujua wewe unaona aaahh.. kawaida tu.
Tazama hilo gari la wagonjwa tunaweza kusema lilikuwa linakwepa foleni kwa sababu maalum, lakini hilo gari la nyuma unaweza kujiuliza lilikuwa likifuata nini kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi. Tukisema hiki ni kipele na kikiachwa kitakuwa jipu ni kosa? Wahusika tuongeze bidii kidogo kupambana na hivi vijipu upele ambavyo dawa yake si ni kuvibinya tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2016


    Ankal, Dawa hapo ni kuwatoza faini ya hali ya juu kila anaye kiuka utaratibu. Kwamfano - Kila kosa shilingi laki moja tena ikalipiwe benki na gari lisitoke mpaka baada ya wiki.

    Ukitoa adhabu kali unayo kula mfuko ilimradi tu pia hiyo adhabu iwe na usimamizi mzuri. Kutakuwa na adabu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2016

    Uenda walikuwa ndugu wa mgonjwa wapo nyuma kuhakikisha wanafika pamoja hospital...Tusifikirie tu negative let think on positive sometimes.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2016

    Ndugu wa mgonjwa wana umuhimu gani kuwahi na kuvunja sheria wakati ambulance ipo? Wao ndo madaktari ama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...