Kiwanda cha bia aina ya serengeti kilichopo
chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi
za kitanzania millioni kumi na sita(16)na Baraza la usimamizi wa mazingira
Nchini(NEMC)baada ya kutokutimiza masharti ya sheria ya mazingira ya
mwaka(2004)na kanuni zake.
Uamuzi huo umefikiwa
baada ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa raisi Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kupata malalamiko kutoka
kwa wanainchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho na kuainisha uchafuzi wa
mazingira yanayowazunguka wananchi hao na kuhatarisha usalama wa afya zao,ambapo ilimlazimu naibu
waziri kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo,huku akiambatana na Wakurugenzi
kutoka Baraza la usimamizi wa mazingira nchini(NEMC)na kujionea uharibifu
huo.
Mh.Mpina ameagiza kiwanda hicho kulipa faini hiyo na
kurekebisha miundo mbinu hiyo ndani ya siku arobaini na tano kusiwepo tena na utiririshaji
maji machafu na yenye kemikali kali za sumu ambayo yanatoa harufu mbaya
inayohatarisha afya za wakazi wa
chang'ombe wilaya ya temeke.
Pia mkurugenzi wa
mazingira Bw. Boniventure Baya ametoa siku saba kwa kiwanda hicho kiwe kimelipa
faini hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kutokana na kwamba
wamekua wakikaidi maagizo yanayotolewa na Baraza hilo la mazingira
nchini(NEMC)na kuwataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo baada ya kukiuka
sheria ya utunzaji mazingira ya mwaka(2004) na kutokutimiza masharti waliyopewa
takribani miaka miwili iliyopita.
Naye mbunge wa Temeke(CUF)
Mh.Abdallah Mtolea alisema kiwanda hicho kimekua na mahusiano mabaya na
wananchi wanaozunguka maeneo jirani na
kiwanda hicho hivyo kupelekea kuwa na mgogoro wa muda mrefu na uongozi kiwandani hapo na kumuomba Naibu waziri kutatua tatizo hilo
ambalo limekua likifanywa kwa makusudi na na uongozi wa kiwanda hicho ilihali
wanajua madhara ya wanayoyapata wananchi.
Aidha kwa upande wake
afisa mazingira wa kiwanda hicho Bw.Simon Peter alipinga vikali tuhuma hizo
ambazo zimeelekezwa katika kiwanda hicho na kusema uongozi wa kiwanda hicho
unafanya kila jitihada ili kuweza kutatua kero hiyo na si kweli kwamba
hawashughulikii tatizo hilo la mazingira jirani na wakazi hao.
Kwa upande wao
wananchi kupitia kwa Bi.Emanuela Peter,walisema hiyo ni kero kubwa sana kwao
ambapo imekuwa ikiwalazimu kuyahama makazi yao hasa wakati wa kipindi cha
masika ambapo maji ya mvua na yale ya kiwanda huchanganyikana na kujaza uchafu
wote majumbani mwao kutoka kiwandani na kuhatarisha afya zao hivyo kuhamia
kwenye nyumba za kulala wageni kwa muda,hivyo wameiomba serikali kuangalia kwa
makini na kuweza kulipatia ufumbuzi.
Vilevile Mh.Luhaga
alifanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha Cement Wazo kilichopo Tegeta
wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,hata hivyo hakuweza kukutana na
kiongozi yeyote wa kiwanda hicho kwa madai kua walikua nje ya mkoa wa Dar es
salaam,aidha Mh.Mpina alitoa tamko la serikali kuwa,serikali ya awamu ya tano haina
uadui na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji kama inavyozaniwa na watu
wengine,bali inachotaka ni kufuatwa kwa Sheria,taratibu na kanuni kama
inavyostahili.
Naibu Waziri Wa nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na
Mazingira Mh.Luhaga Mpina(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa mazingira
wa kiwanda cha serengeti Bw.Simon Peter mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
kiwandani hapo.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina
wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu ni mbunge wa Temeke(CUF)Mh.Abdallah
Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali za kiwandani hapo mara baada ya kufanya
ziara ya kushtukiza.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na
Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho kinavyochuja
maji kwa njia ya kisasa kabisa kwaajiri ya matumizi na uzalishaji kiwandani
hapo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...