Meneja Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. James Mlowe amekabidhi Jumla ya madawati 124 kwa ajili ya shule za Manispaa ya Kinondoni, msaada huo umetolewa na taasisi hiyo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 10,000,000/= yamekabidhiwa kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ali Hapi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ally Hapi (wa pili kushoto) akimshukuru Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 124 kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe iliyopo Kata ya Wazo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
Mkuu wa Wilayaya Kinondoni, Salum Ally Hapi akizungumza katika hafla ya kupokea madawati 124 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...