Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri
Mangi, MAELEZO, Dodoma).
Mbona ukumbi ni wazi; viti vingi havina wabunge?
ReplyDeleteTanzania ilitia saini Maridhiano ya Mkataba wa Paris kuhusu mazingira. Mojawapo ya vipengere vya kulinda mazingira ni kuachana na vyanzo vya nishati vinavyochafua mazingira: matumizi ya gesi, makaa ya mawe na mafuta, ambavyo sasa Tanzania inavipigania kuivusha kwenda katika kundi la nchi za mapato ya kati.
Je, hii haipingani na maridhiano hayo? Wananchi wangependa kusikia wabunge wetu wakilizungumzia suala hili.