Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mwenyekiti wa Yanga aliyemaliza muda wake Yusuph Manji ametoa ahadi kwa wachezaji wake baada ya kuweza kuchukua ubingwa na kuifanikisha timu hiyo kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika.

Manji amekutana na wachezaji hao mara tu baada ya kuwasili kutoka nchini Angola ambako wamefanikiwa kuonyesha uwezo wao kwa kuingia hatua ya 8 bora Afrika.

Akitoa taarifa kutoka kwa Mwenyekiti, Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa wachezaji wote wameandaliwa zawadi watakaporudi utaona utofauti katika muonekano wao.

"Wachezaji wameahidiwa zawadi na Mwenyekiti kwahiyo msije kushangaa utofauti wa muonekano wao pindi watakaporejea uraiani,"amesema Muro. Hata hivyo amesisitiza kuendelea kutoa malalamiko yao kwa bodi ya ligi na TFF juu ya Mechi yao ya fainali ya kombe la FA  siku ya Jumatano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2016

    The mdudu, kama kweli unaitakia mema Yanga ni bora uongee na matajili wenzako ambao nao ni Yanga ili muijengee bonge la uwanja la kisasa kuliko hivyo vizawadi vya msimu ni aibu kubwa sana kwa timu kama Yanga na ukongwe wote huo lakini hata uwanja wa maana haina njooni Uingereza mjifunze nini maana ya Club ya mpira wa Football

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...