Sehemu ya Wakimbiaji wa Mbio za Mwenge, wakiwa tayari kuupokea Mwenge huo ulipowasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016. Zaidi ya vijana 40 waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya Madawa ya kulevwa wanalelewa katika kituo hicho.Picha zote na Othman Michuzi - MMG.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge huo, akiongoza mbio hizo wakati Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukiwasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016.
Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (hayupo pichani) wakati Mwenge huo ulipotembelea kituo hicho Mei 19, 2016.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (kushoto) akimkabidhi Mwenge, Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, wakati wa hafla fupi ya Mwenge huo ulipotembelea kituo chake hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga.






Amani kwa wote, tunashukuru ndugu Bhanji kwa ukarimu wako wa kufungua Sober House ambayo zinawasaidia ndugu zetu wengi waliyoathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.
ReplyDeleteOmbi langu kwako ni kuhusu jina lako kama lilivyoandikwa katika habari husika, aidha muandishi ameliandika kimakosa au ndivyo lilivyo hasa ni Al Karim Bhanji, kwa ulewa wangu naona si vizuri binadamu kuitwa Al Karim kwani hiyo ni sifa ya Muumba pekee, mwanadamu unaweza kuitwa Abdul Karim au Karim bila ya kuweka AL, jina lako likiandikwa kwa kiarabu nadhani wenye kujua kiarabu wanaweza kushituka. Hivyo basi naomba uliangaliye suala hilo.
kwani hakuna aliyekamalika.
Naomba nisieleweke vibaya, hii yote ni katika kunasihiyana na kurekebishana katika mambo yetu ya kidunia na kidini.