Tarehe 23 April, 2016.... ilitimia miaka 400 tangu gwiji wa fasihi, mashairi na tamthiliya, mwandishi maarufu wa Kiingereza, William Shakespeare alipofariki. Mwasisi wa taifa la Tanzania ,Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kutafsiri Kiswahili kazi mbili za Shakespeare :” Mabepari wa Venice” (Merchants of Venice) na “ Julius Kaizari” (Julius Caesar) ... 
Wasanii mbalimbali duniani wamekuwa wakijumuika kutukuza kazi za nguli huyu asiyechuja kwa visa, lugha, nahau, misemo na mada za kila namna. Miongoni mwao ni kundi maalum - “Bards without Borders” (Watenzi Wasio na Mipaka), jijini London. Ndani wamo washairi wa Somalia, Nigeria, Bangladesh, Zimbabwe, Jordan, Colombia, Afghanistan, Bosnia, Ujerumani, Jamaica, Uingereza, India na Tanzania. 
Mwakilishi wa Tanzania ni mwandishi Freddy Macha. Anatumia muziki wa ala mbalimbali ikiwemo Ngoma kumnadi Shakespeare. 
Wakati maonesho mbalimbali yakiendelea kwa kasi Uingereza, Macha ametafsiri kazi zake Shakespeare kwa Kiswahili na pia kuandika tenzi mpya na kikundi hiki. 
Moja ya tukio lililofanyika April 23 , klabu mashuhuri ya Rich Mix, London mashariki, Macha alichanganya mapigo ya Ngoma kadhaa za Kiafrika ikiwepo Sindimba ya Tanzania kutambika na kumsifia gwiji William Shakespeare. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...