Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeanza kusajili Waheshimiwa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; wakati wakiendelea na
kikao cha Bajeti.
Katika Usajili huo NIDA inategemea kusajili wabunge wote ambao hawakuwahi
kusajiliwa awali na kupata vitambulisho vya Taifa, pamoja na kugawa vitambulisho
Wabunge wameonyesha mwamko mkubwa katika kutumia fursa hii adhimu, kwa
kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele kutimiza haki yao ya kikatiba ya
kusajiliwa na kupata kitambulisho cha Taifa; ambacho kimekuwa na faida nyingi
kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Mpaka sasa NIDA imeshatoa zaidi ya vitambulisho zaidi ya milioni 2.5 na kwa sasa
NIDA iko mbioni kuanza usajili kwa kutumia mtaji wa taarifa toka NEC ambapo zaidi
ya wananchi milioni 22 watasajiliwa na kupewa namba ya utambulisho ili kuanza
matumizi mbalimbali.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) akiwa na Afisa Usajili Bw. Surera wakati akipata huduma ya usajili kwenye ukumbi wa Bunge. Katika zoezi hilo mbali na kujaza fomu za maombi ya Utambulisho, pia walichukuliwa alama za kibaiolojia picha na saini ya kielektroniki.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. Saed Kubenea akisaidiwa kujaza fomu za maombi
za Vitambulisho vya taifa na Afisa Usajili Bi. Hadija Bauji.
Mh. Saed Kubenea akisaidiwa na Afisa Usajili Bw. Surera kuchukua alama za vidole
wakati wa hatua ya uchukuaji alama za kibaiolojia.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akisaidiwa kujaza fomu na Meneja Usajili
Vitambulisho vya Taifa, Bi. Julian Mafuru.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...