Afisa wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF Ndg Mohammed Salum akitowa maelezo ya manufaa ya Kujiunga na Uchangiaji wa Hiyari kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano na faida zake kupitia Mfuko huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliodhaminiwa na PSPF.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar Ndg Khamis Rashid, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira kuufungua mkutano huo Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Jengo Sanaa Rahaleo Zanzibar. 
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira akitowa nasaha zake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la Sanaa Rahaleo Zanzibar
 
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Ramadhani Nzori, akizungumza kabla ya kumkaribisha Afisa wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF kuzungumzia umuhimu wa kujichangia kwa hiari katika Mfuko huo kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...