Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imetenga Shilingi bilioni 59.5 katika Bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa.
Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Mahawe aliyetaka kujua ni lini fedha zingetolewa na Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya njia bora ya kutumia fedha hizo.
Dkt. Possi amesema kuwa, fedha hizo zitatolewa mara baada ya kuidhinishwa na Bunge hilo na baada ya kukamilisha taratibu mahususi zinazolenga kuhakikisha uwepo wa tija katika matumizi ya fedha hizo.
Ameongeza kuwa, kuhusu mpango bora wa Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi, Serikali inaendelea kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji wa fedha hizo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya Ujasiriamali.
"Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepewa kazi ya kuratibu utekelezaji wa mpango huo", alisema Dkt. Possi.
Pesa hizo zikiweza kutolewa kila mwananchi aboreshewe makazi yake kulala kusiwe shida wataalamu wa ujenzi wizara husika na vyuo vikuu husika washauri katika kufanikisha hili. Pesa zinazobaki ndiyo tufikirie kuwekeza kwenye upatikanaji wa miundo mbinu ya maji salama ikiwemo kutega maji ya mvua, umeme, gesi na kuboresha kilimo na ujasiriamali, kuna umasikini mwingine hautatoka bila kuwezeshwa na serikali. Serikali ya awamu ya kwanza ili wezesha waliolipiwa shule hata wengine kulipiwa warant za reli kwenda na kurudi shuleni tuunge mkono mpango huu ili uboreshe maisha ya wengi na uchangiwe pia na wanaojiweza waishio mijini.
ReplyDeleteHuu mchakato wote wa kutokomeza umasikini vijijini uwe na ushirikishwaji wa walengwa toka mwanzo. Kushindwa kuwahusisha walengwa kwenye maendeleo kunaweza kusilete matokeo yanayotarajiwa. Ndugu mmoja aliamua kulipia wazazi wake wapate umeme akawafanyia wiring akahakikisha taa zimewaka akalipa luku ya muda mrefu akaondoka. Aliporudi baada ya miezi sita akakuta wako gizani, balbu ziliungua hawakujua jinsi ya kuzibadilisha, somo hapa wananchi washirikishwe katika maendeleo tarajiwa na jinsi ya kuyafanya yawe endelevu.
ReplyDelete