SHIRIKA la ndege la Etihad Airways ambalo ni shirika la kitaifa la UAE, limezindua programu ya simu za iPhone ambayo inasaidia wageni kupangilia na kuratibu safari zao kwa urahisi zaidi kadri ambavyo shirika linavyoendelea kuendana na teknolojia ya kiuvumbuzi ya kupata taswira ya safari.

Wateja wa Shirika la ndege la Etihad watafurahia punguzo la asilimia 10 ya gharama za safari za ndege na wanachama wa programu ya uaminifu ya shirika la ndege la Etihad, watapokea ziada ya maili 250 kwa kila tiketi watakayonunua kupitia programu ya simu kabla ya tarehe 30 Mei 2016. Wale watakao hudhuria katika kituo cha shirika la ndege la Etihad (ME 2310) katika soko la safari la Arabia Dubai kuanzia tarehe 25 – 28 Aprili 2016 wataweza kujaribu vipengele mbalimbali vya programu hiyo na utendaji wake wa kazi.

Programu ya simu ya Shirika la Ndege la Etihad ni rahisi na inafurahisha kutumia, inakupa uwezo wa kuratibu safari zako kikamilifu kwa kutumia mbinu za uvumbuzi wa kisasa zaidi katika teknolojia ya simu za mikononi. Wageni wanaweza kupangilia safari zao katika programu hiyo ikijumuisha kukata tiketi, kufuatiliana na kuangalia hali halisi ya safari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...