
Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rshid Ali Juma akizungumza na wafanyakazi na wananchi walioshiriki maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazi mmoja Zanzibar.

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya kudumu ya sanaa katika maadhimisho ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdalla akimuonyesha Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo sanaa ya ufumaji kofia za asili ya Zanzibar katika maonyesho ya sanaa yanayofanyika makumbusho ya Mnazimmoja.

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akiangalia kazi ya ubunifu iliyofanywa na msanii Naaman Ali Khamis wa kwanza (kulia) anaetumia majani makavu ya migomba.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...