Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Saraha Kibonde Msika, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Makete hivi karibuni.
Waelimishaji kutoka SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) na Bw. David Lyanga (kulia mbele), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Ualimu Hagafilo Njombe.
Ofisa kutoka SSRA, Bw. David Lyanga akitoa mada kuhusu Hifadhi ya Jamii wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na SSRA, mkoani Njombe hivi karibuni.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa SSRA, Bw. Peter Mbelwa akitoa maelezo kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii wakati wa Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), iliyofanyika kwa Wanachuo na Wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Binza, kilichopo Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu hivi karibuni.
Ofisa uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Agnes Lubuva akitoa mada ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Binza kilichopo Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, hivi karibuni.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...