TAWI la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) la Makao
Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA-HQ), limepata
viongozi wake wapya katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi
wa Transit uliopo katika jengo la Kiwanja cha Ndege cha Zamani (TBI).
TAA ni wakala wa Serikali iliyoanzishwa tarehe 29 Novemba 1999 kwa Tangazo
la Serikali Na.404 la mwaka 1999 chini ya kifungu cha 3 cha Sheria Na. 30 ya
mwaka 1997 ya Wakala wa Serikali. Wakala hii ilirithi majukumu ya iliyokuwa
Idara ya Viwanja vya Ndege (Directorate of Aerodromes) chini ya Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi, ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 3 Desemba 1999.
Viongozi hao wamepatikana baada ya uliokuwepo kumaliza muda wao, na
waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mkuu wa TUGHE
Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango, ni pamoja na Mwenyekiti Bw.
Nasib Elias aliyezoa kura zote 28, baada ya kutokuwa na mpinzani, huku katibu
mkuu akichaguliwa Bi. Aziza Kipande aliyepata kura 15 akimshinda Bi. Caroline
Mntambo aliyepata kura 13.
Wajumbe watatu ambao ni Bi. Mwanaisha Omari, Bw. Joel Mwakamele na Bi.
Frida Omari walipitishwa bila kupingwa na wajumbe waliotoka idara mbalimbali
za TAA HQ.
Naye Bi. Irene Sikumbili alipata kura zote 14 za wanawake na kuchaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake na Katibu Mkuu wake ni Bi. Mwanahawa
Mdee aliyepata kura 11 akimshinda Bi. Kipande aliyepata kura tatu.
Walioshinda katika nafasi ya ujumbe katika kamati hiyo ni Bi. Glory Mollel na Bi.
Pendo Pascal; wakati Bi. Mntambo ameukwaa uweka hazina na Bi. Magreth Mushi
ni mwakilishi wa vijana, huku hakukuwa na mwakilishi wa walemavu kutokana na
kutokuwa na mlemavu.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Bw. Abdi Mkwizu alipata nafasi ya
kuwapongeza viongozi wateule wa TUGHE na kuwaahidi ushirikiano mzuri
kutoka upande wa mwajiri.
Katika kutoa neno la shukrani kwa wajumbe, Mwenyekiti Bw. Elias aliwashukuru
wajumbe wote kwa kuonesha imani yao ya dhati kwake na kuwaahidi kuendeleza
mshikamano na mahusiano mema yaliyojengwa na uongozi uliomaliza muda wake
baina ya wafanyakazi na mwajiri, lakini pia baina ya wafanyakazi wenyewe.
Bw. Elias pia ameahidi kuhakikisha wafanyakazi ambao si wanachama wa
TUGHE wanajiunga na chama hiki kwani kina manufaa makubwa kwao
yakiwemo ya kutetewa pindi mfanyakazi anapokuwa kwenye matatizo na mwajiri
wake .
Naye msimamizi, Bw. Kadyango ambaye aliukabidhi uongozi mpya katiba,
aliwashukuru wajumbe wote kwa kumaliza zoezi la uchaguzi kwa amani na
kusisitiza kuwa na ushirikiano mzuri na mwajiri, kudumisha uhusiano mwema
kazini kati ya waajiri na waajiriwa, kudumisha uhusiano mwema baina ya
wafanyakazi wao kwa wao, kusimamia uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi na
hali bora za kazi, ili kufikia malengo.
Viongozi wapya wa TUGHE tawi la TAA Makao Makuu, wakiwa katika picha ya pamoja.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...