Na Woinde Shizza,Arusha

Vijana wametakiwa kujijengea tabia ya kushiriki michezo mbalimbali kila mara badala ya kujiingiza katika makundi mabaya ya wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kitu ambacho kinawaaribia mfumo mzima wa maisha yao.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwandaaji wa Tamasha vijana la mpira wa miguuu linaloendeshwa kwa mfumo wa ligi ya mpira wa miguu linayowashirikisha vijana kutoka katika kata ya sakina .

Alisema kuwa yeye kama mama anaumia sana kuona vijana wanakaa mitaani na kujiingiza katika vitendo mbalimbali mbali ikiwemo wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevywa ivyo ameamua kuanzisha ligi hii ili kuwasaidia vijana wengi kushiriki na kuachana na makundi .

"unajua pia michezo ni ajira hivyo nimeona ni vyema mimi kama mama kiongozi wa watoto nianzishe ligi hii ya mpira wa miguu ili awa vijana wetu waweze kushiriki,kujifunza na pia ule mda walikuwa wanatumia kwenda kuangaika uko mtaani na kutumia madawa ya kulevywa watakuja apa watashiriki michezo "alisema Neema

Aidha alibainisha kuwa ligi hii aitaishia kipindi hichi kwani itakuwa endelevu na ameamua kuanza na watoto wa kiume kwa kuanzisha mpira wa miguu lakini pia anania yakuanzisha ligi ya wanawake ya mpira wa pete ili pia kuwawezesha watoto wakike nao kujitokeza na kujifunza kwani michezo pia ni ajara pamoja na afya.

Kwa upande wake Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku hii ya uzinduzi wa mashindano hayo Emanuel Makongoro alisema kuwa amefurahishwa sana kuona jinsi vijana walivyojitokeza kushiriki ligi hiii kwani wametambua umuimu wa michezo katika afya zao.

Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Emanuel Makongoro akiwa amnawapa mawaidha wachezaji kabla ya mechi kuanza
Mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa tamasha la vijana akiwa anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha hilo
Wachezaji wakiendelea kusakata kandanda ndani ya kiwanja cha ngarenaro mkoani arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...