• Wawezeshwa vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni tano.

Airtel Tanzania inaendeleza dhamira yake ya kuendelea kuwashika mkono vijana hapa nchini  ambapo mwishoni mwa wiki hii kupitia mpango wake wa kutoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha, uliweza kuchagua vijana wawili walioweza kuelezea na kuwakilisha changamoto wanazozipata katika biashara wanazozifanya mbele ya jopo la washauri ambao leo hii wamekabidhiwa  vitendea kazi vyenye dhamani ya shilling milioni 5  ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

Akizungumza wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo, Meneja wa Airtel huduma kwa Jamii Hawa Bayumi alisema "baada ya kufanya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali wiki chache zilizopita na kuweza kufikia vijana zaidi ya 300 jijini Dar Es Salaam  waliojitokeza na kuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira na na uwezo wa kujenga fursa nyingine. Leo hii tupo hapa kuwawezesha hawa walioonyesha bidi zaidi”

“Na siku hiyo ilikuwa ni siku ya faraja kwani vijana waliweza kujifunza mambo mengi sana na mwisho wa siku waliweza kuelezea na kuwasilisha biashara zao mbele ya jopo la washauri na ulikuwa uamuzi mgumu sana lakini mwisho wa siku tuliweza kupata vijana wawili bora walioweza kushinda nyoyo za jopo la washauri hao, ambao leo  hii tupo hapa kwajili ya kuwakabidhi vifaa vyao ili waweze kwenda  kukabiliana na changamoto walizonazo katika biashara zao. "

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Stephen Gimase (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiangalia vifaa alivyokabidhiwa na Airtel FURSA kwa ajili ya kuboresha biashara yake ya kutengeneza mashine za kutengenezea vifaranga vya kuku, Kushoto ni Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi 
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (2 Kushoto) akimkabidhi Theresia Maliatabu (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” vifaa vyakuboresha biashara yake ya uchoraji ikiwemo meza ya kuchorea na kompyuta ya kisasa. Kijana huyu Aliyechaguliwa kutoka kwenye mafunzo ya biashara ya ujasiriamali  ya Airtel FURSA yaliyofanyika Dar es Salaam wiki chache zilizopita. Akishuhudiwa na mama yake mzazi Judith Benedicto (Katikati) na mama mkubwa Salome Benedicto (Kulia) pamoja na Afisa mauzo wa Airtel katika hafla iliyofanyika Mbagala kuu, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...