Na Woinde Shizza wa 
 Globu ya Jamii, Arusha.
Kusimamishwa kwa shindano la umrembo Tanzania (Miss Tanzania ) kwa mwaka mmoja imekuwa ni changamoto kubwa kwa waandaaji wa shindano hilo, kwani warembo wengi wamesahau mambo kibao ndani ya mashindano hayo.
Hayo yamebainishwa na muaandaaji wa shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha kutoka katika kampuni ya Tour Visual Entertainment, Penda Simwita wakati akiongea nasi  katika kambi ya kumuandaa Miss Arusha 2016.
Alisema kuwa kwa upande wake shindano hilo limekuwa gumu kidogo, kwani warembo wengi walibweteka na kujisahau kuwa kuna shindano kama hili kwa mwaka huu, hivyo ilimlazimu kutembelea katika vyuo mbalimbali vya hapa mkoani Arusha kwa ajili ya kuwasaka warembo watakaoshiriki shindano hili.
"Pamoja na kuwatafuta,tumefaniwa kuwapata warembo wazuri wenye sifa na naamini wataweza kutetea taji la Miss Tanzania,kwani wana uwezo na kizuri zaidi najiamini naweza kuwaandaa maana hata mrembo ambaye anashikilia taji sasa hivi alitoka mkoa wa Arusha" alisema Mwandaaji huyo.
Mmoja wa warembo wanaoshiriki shindano hilo ,Maurine Ayubu alieleza hisia zake za kufurahi kushiriki shindano hilo,alisema kuwa ana uwezo wa kufanya vizuri,na kwamba ana uhakika wa kufanya vyema kwa sababu sifa zote za kuwa mrembo wa Mkoa wa Arusha anazo na kwamba anaamini atatetea taji la Miss Tanzania libaki Arusha kama linavyoshikiliwa kwa sasa na mrembo wa Tanzania Lilian kamazima

Jumla ya warembo 17 kutoka katika mitaa mbalimbali na wilaya mkoani hapa wanatarajiwa kupanda jukwaani mapema May 28 mwaka huu katika ukumbi wa Hotel ya Naura Spring kwa ajili ya kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha ambaye atawakilisha mkoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania na tukumbuke mpaka hivi sasa taji hilo la mrembo wa Tanzania linashikiliwa na mrembo kutoka mkoa wa Arusha Lilian Kamazima .

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha wakiwa katika pozi
warembo hao wakiwa wanacheza hii ikiwa ni moja ya mazoezi yao wanayoyafanya ndani ya ukumbi wa hoteli Naura Spring Arusha ambapo wameweka kambi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...