Frank Mvungi –Maelezo.

Wanaharakati na wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, wametakiwa kuacha kuupotosha umma juu ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali hiyo chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam leo na Afisa Habari wa CZI- information And Media Consults Co. Ltd, Augustino Matefu wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano.Alisema Serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio makubwa katika sekta ya ukusanyaji mapato, elimu, miundombinu, afya na kujenga uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.

Hivyo alitoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano na kuwapuuza wanaharakati na wanasiasa hao wanaunga mkono wale wasioitakia mema Tanzania na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla.Alisema katika sekta ya mapato, Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miezi saba iliyopita imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 900 kwa mwezi kabla ya utawala wake hadi shilingi trilioni 1.5 kwa sasa.

“Rais wa awamu ya tano ameondoa michango yote ya shule za msingi na Sekondari ambayo ilikuwa kero kwa wazazi na wananchi kwa ujumla” alisisitiza Matefu Katika mpango wa elimu bure Matefu alibainisha kuwa umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na elimu ya msingi na ile ya Sekondari.

Aliongeza kuwa Rais Magufuli amejenga Barabara ya Mwenge hadi Moroko kwa Fedha za ndani hali inayoonyesha kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.Alisema hata Hosipitali ya Taifa Muhimbili Kupatiwa vitanda vya kutosha na hivyo kuondoa tatizo la msongamano katika wodi ya wazazi na kwa sasa wagonjwa wanalala kwenye vitanda.

“Mambo mengine yaliyofanywa na Serikali katika kipindi hiki yanalenga kuinua maisha ya wananchi wa chini ikiwemo kujenga mazingira mazuri yatakayowezesha shughuli za uzalishaji kuongezeka ili kuinua hali ya maisha ya wananchi” alisema Matefu.Kujengwa kwa utamaduni wa uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma ni moja ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano ambapo sekta ya utumishi wa umma imeonesha mabadiliko makubwa katika uwajibikaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2016

    Yako mengi mazuri yaliyofanyika kwa kipind kifupi. Hili la kurudisha utendaji kazi wenye maadili katika sekta ya umma, kufuata taratibu na kuhakikisha mapato ya serikali yanatumika vizuri ni kitu ambacho matokeo yake na ufanisi yanaonekana wazi yaendelee kuboreshwa ili wengi wafanikiwe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2016

    Mtu mmoja aliwahi sema kuna watu ambao kazi Yao ni kupinga na kubeza chochote kile kinachofanywa na Serikali. Watu hao leo hata Magufuli afanye Maajabu Kama ya kutembea juu ya maji wangesema katembea kwa vile hawezi kuogelea!!! Serikali iwasikilize wapinzani na wanaobeza. Isiwapuuze lakini ilenge tu kutimiza ahadi zake kwa wananchi kwani mwishoni wao ndo waamuzi. Mengine ni upumbavu tu.

    ReplyDelete
  3. Hawa watakuwa ukawa tu ndiyo wanaopinga juhudi za serikali. Ni akili mbaya tu walionazo wakiongozwa na mbowe sugu na lissu washindwe na waregee kabisa!!

    ReplyDelete
  4. Hawa watakuwa ukawa tu ndiyo wanaopinga juhudi za serikali. Ni akili mbaya tu walionazo wakiongozwa na mbowe sugu na lissu washindwe na waregee kabisa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...