
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza (Minister of State for International Development) , Justine Greening katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje , Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Kikanda naKimataifa, Augustine Mahiga na watatu kushoto ni Jaji Mkuu,Mohamed Othman.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May12, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Norway,Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg (kulia) katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. anne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...