Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Ikicheza ndani ya dimba la Centuary Link Field, Seattle Washington,timu ya Argentina bila nyota wake na mchezaji bora mara 5 wa dunia Lionel Messi iliigalagaza Bolivia kwa jumla ya mabao 3-0. 

Argentina imetinga robo fainali kwa kujikusanyia pointi 9 baada ya kushinda mechi zake zote tatu kwenye kundi D. Mabao ya washindi yalipatikana katika kipindi cha kwanza yaliofungwa na Erick Lamela kunako dakika ya 12, Ezequiel Lavezz dakika ya 15 na Victor Leondro Cuesta katika dakika ya 32.

Lakini mchezo huu ulitawaliwa zaidi na ubabe wa hapa na pale kiasi cha mwamuzi V.Carrillo kumwaga kadi za njano kwa wachezaji 5 ambao ni Ever Banega na Victor L.Cuesta(Argentina), Edward Zenteno, Jhasmany Campos na Alejandro Melean(Bolivia).Argentina atapambana na Venezuela kwenye robo fainali.
Nayo Chile imemaliza mechi zake za kundi D kwa kishindo baada ya kuifunga Panama mabao 4-2 kwenye mchezo mkali na wa kusisimua wa funga nikufunge uliopigwa kwenye dimba la Lincon Financial Field, Philadelphia na kuamuliwa na mwamuzi R. Zambrano.

Eduardo Vargas na Alexis Sanchez waliifungia Chile mabao mawili kila mmoja (Eduardo dakika ya 15 na 43) huku (Sanchez dakika ya 50 na 80) wakati mabao ya Panama yalifungwa na Miguel Camargo dakika ya 5 na Abdiel Arroyo kunako dakika ya 75..

Robo fainali zitaanza kesho kwa mchezo kati ya MAREKANI vs EQUADOR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...