Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kwenye vitabu ambavyo ni muongozo wa kazi kwa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.Katika hotuba yake, Waziri Ummy ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
kuwekeza katika viwanda vya dawa hasa kwa zile dawa za msingi, kwani utaboresha sana upatikanaji wa huduma, utapunguza malalamiko
kwa wanachama wake, utaongeza ajira na pia kupunguza
matumizi ya fedha chache za kigeni kwa ajili ya kununulia dawa
hizo nje ya nchi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda, akitoa shukrani zake baada ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...