NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 

SAKATA la mgogoro wa ardhi kwa wananchi wa kijiji cha mwavi kata ya Fukayosi kilichopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na mwekezaji ambaye ni mkorea limechukua sura mpya baada ya mkuu wa Wilaya hiyo kuamua kuliingilia kati suala hilo kwa lego la kurudisha hali ya amani na utulivu pamoja na kumaliza tofauti zilizokuwepo. 

Mgogoro huo ambao umeonekana kuwa na mvutano mkubwa kutokana na mwekezaji huyo kupatiwa eneo lenye ukumbwa wa hekari 231 za serikali ya kijiji pasipo kuwashirikisha wananchi wenyewe kitu ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa kutoelewana kati ya wanakijiji na mwekezaji huyo. 

Akizungumzia kuhusina na sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kwamba baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mwekezaji huyo alipewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji,ambapo kwa sasa wamekubaliana naye hekari 131 zirudishwe kwa wananchi wenyewe na yeye abakiwe na hekari 100 tu. 

“Jamani wananchi wa kijiji cha mwavi mimi baada ya kuniletea malalamiko hayo nimeyafanyia kazi kwa kina kabisa ambapo nimekutana na mwekezaji huyo tumeongea naye juu ya suala hilo na amekubali kuzirudisha hekari 131za ardhi kwa wananchi nayeye atabakiwa na hekari 100 kwa ajili uwekezaji katika eneo hilo ambapo atajenga kituo cha kilimo, shule, zahanati pamoja na mambo mengine hivyo tuwe watulivu tumwone kama ataziendeleza kama tulivyokubaliana. 

Alisema kwamba serikali ya awamu ya tano ambayo inangozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli itahakikisha kwamba inaleta mabadiliko chanya kwa kuzingatia usawa bila ya kuwa na uonevu wowote ule hasa katika masuala ya ardhi ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kubwa katika Wilaya ya bagamoyo na maeneo mengine, na kuahidi kushirikiana nao mambo yote ya kimaendeleo. 
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha mwavi kata ta Fukayosi Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika mkutano maalumu na kutatua sakata la mgogoro wa ardhi baina yao pamoja na mwekezaji Mkorea, ambaye amepokonywa hekari 131 na zimerudishwa kwa wananchi wenyewe.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wawekezaji hao ambao ni wakorea wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...