Daktari Mshauri Mwandamizi wa Magonjwa ya Moyo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis, Dkt. Harun Nyagori amealikwa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo Duniani unaofanyika nchini Mexico.
Dkt. Nyagori ambaye alikuwa Mtanzania wa kwanza Mwaka jana kupata tuzo ya Kimataifa nchini Uingereza na kutambuliwa na Shirikisho la Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo Barani Ulaya, ameshiriki Mkutano huo ambao mada kuu inayojadiliwa ni kupunguza kasi ya vifo vya Wagonjwa wanaokufa kwa maradhi ya Moyo hasa kusini mwa nchi za kusini mwa Africa ikiwemo Tanzania kwa kutumia teknolojia ya kisasa na namna ya kuwafikia hao wagonjwa.
Tanzania sasa imepiga hatua kwa kufanya upasuaji wa wagonjwa wa moyo wenye matatizo makubwa yaliyohitaji kutibiwa nje ya nchi, ila sasa huduma hizo zinapatikana Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...