Assalaam alaykum,
Aisha Sururu Foundation ina furaha kuwaalika kwenye fainali ya mashindano ya mwaka 2016 (1437 AH) ya kuhifadhi Qur’an tukufu itakayofanyika Jumapili ya tarehe 19/06/2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es salam, ambapo vijana wanawake na wanaume watakaoshiriki katika mashindano haya watapigania nafasi zao za kwanza kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur’an katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Mashindano ya kuhifadhi Qur’an ya mwaka huu yatakuwa ni mashindano ya kumi na nne (14) tangu mashindano ya kuhifadhi Qur’an yanayoandaliwa na Aisha Sururu Foundation yaanzishwe, Alhamdulillah.
Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 24 ya Tanzania pamoja na visiwa vya Zanzibar, Unguja na Pemba, kwa nia ya kuwashajiisha watoto kuhifadhi Qur’an katika viwango vya juu vya kuisoma Qur’an tukufu.
Kauli Mbiyu ya Mwaka Huu: Tuwathamini Waalimu Wetu wa Qur’an Tukufu, Tupate Radhi za Mola Wetu Ra’ufu.
Tukio: Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu.
Tarehe: 19/06/2016.
Ukumbi: Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam, Tanzania.
Wakati: Saa 2 Asubuhi Mpaka Saa 8 Mchana (8am – 2pm).
Mgeni wa Heshma: Mheshimiwa Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu.
Shukran.
Wabillahi Tawfeeq,
AISHA SURURU FOUNDATION

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...