Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe
akimkabidhi Mratibu Mkuu wa ICGLR, Balozi Samuel Shilukindo kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje (Mwenyekiti) vitendea kazi wakati akizindua
Kamati ya Kimataifa ya Kusimamia Utekelezaji wa Mpango wa ICGLR
Tanzania jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe
(mbele) na kulia kwake aliyesimama ni Mratibu Mkuu wa ICGLR, Balozi
Samuel Shilukindo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje akisoma hotuba wakati
wa uzinduzi na wengine katika picha ni wanakamati.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe
(mbele) na wajumbe wa kamati hiyo wakimsikiliza Kaimu Kamishna wa
Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ally Samaje (aliyesimama)
akitoa mada katika uzinduzi uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara jijini
Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe
wa nne kutoka kulia akiwa pamoja na Kamati ya Kimataifa ya Kusimamia
Utekelezaji wa Mpango wa ICGLR Tanzania na Wajumbe kutoka Wizara
ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza
uzinduzi wa Kamati hiyo.
Na Rhoda James
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia
madini Profesa James Mdoe kwa Niaba ya Katibu Mkuu, Profesa Justin
Ntalikwa tarehe 22 Juni, 2016 alizindua Kamati ya Kimataifa ya Kutekeleza
Mpango ujulikanao kama International Conference on the Great Lakes
Regional Initiative Against Illegal Exploration of Natural Resources (ICGLK-
RINR) katika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Profesa Mdoe alisema kuwa lengo la Mpango wa ICGLR- RINR ni kuweka
mfumo wa usimamizi wa uchimbaji, uchenjuaji, usafirishaji na uuzaji wa
madini ili kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanywa kihalali na hazitumiwi
na vikundi au watu wanaohusika katika kuendeleza migogoro na vita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...